
Maafisa wa DCI wamewakamata washukiwa watatu wanaoaminika kumuua mwanafunzi wa chuo kikuu cha Egerton mwaka jana.
Maafisa hao wamesema watatu hao Diana Njeri, Tamar Wabora na Eric Maingi walimuua mwanafunzi huyo wa miaka ishirini na mwili kisha kuutupa mwili wake katika Mto Subuku, ulioko Njoro Nakuru.
Wamesema uchunguzi wao umebainisha kwamba mshukiwa wa kwanza, Diana Njeri alikuwa katika eneo ambapo mwili ulipatikana usiku wa tarehe 7, Desemba mwaka jana.
Aidha Njeri, Wambora na Maingi walipatikana na kadi za simu mia saba ishirini na mbili na simu saba za rununu.
Hayo yanajiri huku uchunguzi dhidi ya watu waliowasaidia kuutupa mwili huo mtoni ukiendelea.
Washukiwa watafikishwa katika Mahakama ya Nakuru Jumatatu ijayo kujibu mashtaka dhidi yao.
Share this: