×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanafunzi 258 wa Makueni Boys wafukuzwa kwa kukataa kunyoa ndevu

Wanafunzi 258 wa Makueni Boys wafukuzwa kwa kukataa kunyoa ndevu

Usimamizi wa Shule ya Wavulana ya Makueni unatarajiwa kutathmini uharibifu shuleni humo baada ya watahiniwa wa kidato cha nne kurusha mawe wakikataa kunyolewa.

Tayari wanafunzi 258 wa kidato cha nne katika shule hiyo wametumwa nyumbani baada ya kuzua rabsha jana jioni wakikataa kunyolewa.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Raphael Katana amesema wanafunzi wengine walikubali kunyolewa jinsi ilivyo kawaida yao kunyolewa kila mwezi lakini ilipofika zamu ya wale wa kidato cha nne, wakakataa na kuanza kurusha mawe.

Maafisa wa Polisi wa Makueni wamekesha katika shule hiyo ili kuhakikisha hali ya utulivu inarejeshwa, kwani walikuwa wamemjeruhi mwalimu mkuu kwa mawe japo alitibiwa.

Share this: