×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 yaongezeka nchini

Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 yaongezeka nchini

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Ikiwa ni siku ya 339 tangu virusi vya korona kuripotiwa nchini, idadi ya maambukizi imeendelea kupanda katika kipindi cha siku 4 zilizopita, ikiwa ni watu zaidi ya mia moja kila siku.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, watu wengine 283 wameripotiwa kuambukiwa virusi hivyo chini ya saa 24 zilizopita kutokana na sampuli 4,822 na hivyo kufikisha jumla ya 103,615 idadi ya wa maambukizi nchini huku kiwango cha maambukizi kikiwa 5.8.

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa idadi ya maambukizi huku wagonjwa wengine 66 wakiripotiwa kupona, 51 miongoni mwao wakiwa waliokuwa wakitibiwa nyumbani huku waliosalia wakiwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, wagonjwa wengine 6 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo wa Covid-19 na hivyo kufikisha 1,807 jumla ya idadi ya vifo nchini.

Share this: