×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Halakhe Waqo ahusishwa na sakata ya KEMSA

Halakhe Waqo ahusishwa na sakata ya KEMSA

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC Halakhe Waqo ameagizwa kufika mbele ya Kamati ya Uwekezaji ya Bunge la Kitaifa kuhojiwa baada ya kuhususishwa na sakata ya kupotea kwa fedha za kulikabili janga la korona katika Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa na Vifaa vya Matibabu, KEMSA baada ya kuhusishwa na sakata hiyo.

Mfanyabiashara Zubeida Namlondo aliyehojiwa na kamati hiyo amesema kwamba Halakhe alimfadhili kupata mkopo wa benki wa shilingi milioni 175 ili kununua maski na kuzisambazia KEMSA kupitia kwa kampuni ya Aszure licha ya kwamba biashara yake inahusu uuzaji wa fenicha. Kamati hiyo chini ya uwekenyekiti wa Mbunge wa Mvita, Abdul Swahmad Nasir imebaini kwamba Zubeida alilipwa shilingi milioni 350 ili kusambaza maski hizo.

Imebainika kwambwa kampuni hiyo ilisambaza sanduku elfu hamsini za maski ambapo kila sanduku liliuzwa kwa shilingi mia sita tisini. Zubeida hata hivyo hakufafanua namna alivyojuana na Waqo akisema alisahau walivyojuana.

Kamati hiyo ya Uwekezaji inalenga kubaini iwapo Waqo ndiye mmiliki wa Kampuni ya Aszure na alimtumia Zubeida ili kumsadia kupata tenda ya KEMSA. 

Share this: