×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gari la Naibu Gavana wa Kisii lateketezwa

Gari la Naibu Gavana wa Kisii lateketezwa

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Naibu Gavana wa Kisii, Joash Maangi anatarajiwa kurekodi taarifa katika Kituo cha Polisi cha Narok kufuatia ajali iliyotokea Jmatano jioni ambapo gari lake lilimgonga mhudumu wa bodaboda pamoja na mwanawe ambao walifariki dunia papo hapo.

Kamanda wa Polisi kwenye Kaunti ya Narok, Kizito Mutoro amesema anatarajiwa kwamba gavana huyo atafanyiwa uchunguzi wa kiafya kwanza kabla ya kurekodi taarifa. 

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na mbili unusu katika eneo la Tegero karibu na Kituo cha Kibiashara cha Ololung'a ambapo inaarifiwa kwamba mhudumu huyo wa bodaboda aligongwa pamoja na mwanawe mwenye umri wa miaka minane walipokuwa wakivuka barabara. 

Maangi alikuwa katika gari hilo pamoja na walinzi wake wawili japo hawakujeruhiwa. Ajali hiyo ilichangia kuteketezwa kwa gari la gavana huyo na wananchi waliojawa na ghadhabu. Kamanda wa Polisi Kizito Mutoro amesema gari hilo aina ya Prado liliteketea kabisa

Share this: