
Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi mjini Eldoret imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana mapema leo kulalamikia uongozi mbaya.
Kupitia barua iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Uasin Gishu, Mbaga Gitonga wazazi wameagizwa kuwachukua wanao kabla ya siku ya leo kukamilika.
Hatua hii imechukuliwa baada ya kikao cha bodi ya usimamizi wa shule hiyo na viongozi wa idara ya elimu.
Wanafunzi hao waliandamana kushinikiza kuondolewa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kwa madai kwamba amekuwa akiwakandamiza, vilevile kuwakandamiza walimu pamoja na wafanyakazi na kuiongoza shule kwa njia isiyofaa.
Share this: