×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti za Busia na Siaya zatajwa kuwa zinazoongoza kwa vifo vya Malaria

Kaunti za Busia na Siaya zatajwa kuwa zinazoongoza kwa vifo vya Malaria

Serikali imezitaja Kaunti za Busia na Siaya kuwa na idadi ya juu ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amelitaja janga la Korona kuwa lililotatiza pakubwa vita dhidi ya malaria.Kagwe amezungumza wakati wa uzinduzi  wa baraza la kukabili ugonjwa huo nchini.

Kagwe amesema baraza hilo ni la tano kuanzishwa Barani Afrika na litasaidia pakubwa kubuni sera za kukusanya rasilimali za kukabili Malaria.

Waziri Kagwe amesema inasikitisha kwamba vifo kutokana na malaria viliongezeka pakubwa mwaka 2019 kinyume na ilivyotayarijiwa ambapo watu elfu tatu themanini na wanane walifariki dunia. 

Share this: