×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 10 waorodheshwa kuwania wadhifa wa Jaji Mkuu kumrithi Maraga

Watu 10 waorodheshwa kuwania wadhifa wa Jaji Mkuu kumrithi Maraga

Watahiniwa 10 wameorodheshwa kuwania wadhifa wa Jaji Mkuu nchini kabla ya shughuli ya mchujo kuanza rasmi mwezi Aprili mwaka huu.

Aidha, watahiniwa wengine 9 wanaolenga kutwaa wadhifa wa Jaji wa Mahakama ya Juu vilevile watachujwa wakati huo.

Kwa mujibu wa Tume ya Huduma za Idara ya Mahakama, jumla ya wagombea 13 walituma barua za maombi ya kumrithi David maraga ambaye alistaafu mwezi uliopita.

Miongoni mwa waliotuma barua za maombi ni; Said Chitembwe, Prof Patricia Mbote, majaji Martha Koome, Marete Njagi, Philip Murgor,  Nduma Nderi, Fred Ngatia,  William Ouko, Dr Wekesa Moni na Alice Yano.

Ikumbukwe kuwa Majaji wote wa Mahakama ya Juu ambao wanahudumu kwa sasa walikosa kutuma barua za kujaza wadhifa huo akiwemo Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Share this: