×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila asalia pekee baada ya wenzake wa NASA na KANU kubuni muungano na kumwacha nje

Raila asalia pekee baada ya wenzake wa NASA na KANU kubuni muungano na kumwacha nje
Miungano ya kisiasa kabla ya mwaka elfu 2022 inaendelea kujitokeza huku sasa ikidhihirika kwamba huenda Kinara wa ODM, Raila Odinga atasalia pekee miongoni mwa waliokuwa viongozi wa NASA iwapo atataka kuwania urais mwaka huo.
 
Hapo jana Viongozi wa Vyama vya Ford Kenya, ANC, Wiper na KANU wametangaza kubuni ushirikiano wa kisiasa kuelekea uchaguzi huo.
 
Wakizungumza katika Eneo Bunge la Kabuchai, Kaunti ya Bungoma wakati wa kumpigia debe mwaniaji ubunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga, vinara wa vyama hivyo wamesema muungano huo utawaleta pamoja Wakenya wote.
Ikumbukwe katika siasa zizo hizo za mwaka elfu 2022 kunatarajiwa mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto na mirengo ya wagombeaji wengine kama vile Dr Mukhisa Kituyi, Dr Alfred Mutua, Prof Kivutha Kibwana miongoni mwa wengine.
 
Mirengo hiyo pia itategemea iwapo mchakato wa BBI utafanikiwa ili kuwa na nydhfa zaidi ambazo wanaowania urais watategemea ili kuwaahidi viongozi tajika ili kuvutia uungwaji mkono kwenye maeneo mbalimbali. Iwapo BBI itakuwapo kutakuwa n nyadhfa za Urais, Naibu, Waziri Mkuu na manaibu na hata maspika.

Share this: