
Marufuku ya kuwa nje iliyotangazwa katika Kaunti za Baringo na Turkana imechapishwa rasmi kwenye gazeti la serikali. Kwa mujibu wa ilani iliyochapishwa, wakazi hao hawatakiwa kuwa nje kuanzia saa kumi na mbili joini hadi saa kumi na mbili asubuhi kwa siku 30.
Maeneo yakayoathirika ni Turakana Mashariki na Tiaty. Marufuku haya yanamaanisha kwamba hakutaruhusiwa mikutano wala shughuli zozote katika kipindi hicho
Wiki iliyopita, Mbunge wa Tiaty alitiwa mbaroni akihusishwa na vita vya mpakani nawizi wa mifugo hasa kwenye eneo la Kapedo. Hata hivyo aliachiliwa baadaye na kuagizwa kufika katika ofisi za Idara ya Upelelezi katika Kaunti ya Nakuru hapo kesho ili kuendeleza uchunguzi.
Serikali inaendeleza operesheni kali kwenye eneo hilo kufuatia kuuliwa kwa afisa wa kitengo cha juu katika kitengo cha GSU vilevile vifo kadhaa vya raia na wizi wa mifugo.
Share this: