
Kundi la vijana limetatiza kwa muda mkutano wa Kinara wa ODM Raila Odinga wa kupigia debe mchakato wa BBI kwenye eneo la Githurai.
Kundi hilo la vijana takriban 50 lilikuwa likiimba nyimbo za kumpigia debe Naibu wa Rais, William Ruto na kurusha mawe kwa mkusanyiko uliokuwapo kabla ya makabiliano makali kuzuka baina ya kundi linalomuunga mkono Raila vilevile polisi nao.
Hata hivyo, baadaye Raila aliendelea kuwahutubia wakazi wa eneo hilo baada ya kufanya mkutano na wafanyabiashara wa Githurai.
Share this: