
Mtoto mchanga wa umri wa miezi minne ni miongoni mwa watu 130 ambao ni wa hivi punde kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya korona huku mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 88.
Sampuli zilizopimwa katika kipindi hicho ni elfu nne mia tisa kumi na nane kiwango cha maambukizi ni cha asilimia 2.6 kulinganisha na jana ambapo kilikuwa asilimia 2.5. Miongoni mwa walioambukizwa, 115 ni Wakenya huku 15 wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.
Wanaume walioambukizwa ni 88 huku wanawake wakiwa 42. Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi mapya ambapo watu 66 wamethibitishwa kuambukizwa ikifuatwa na Taita Taveta watu 18 na Mombasa 9.
Mtu mmoja zaidi amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 na kufikisha elfu moja ia saba hamsini na mmoja idadi jumla ya waliofariki dunia. Aidha watu sitini na sita wamepoba ugonjwa huo ambapo 42 walikuwa wakihudumiwa nyumbani n a 24 hospitalini. Idadi jumla ya waliopona sasa imefikia elfu themanini na tatu, mia sita tisini na mmoja.
Share this: