
Msajili wa Idara ya Mahakama ametangaza kwamba Mahakama ya Milimani itafungwa kuanzia siku ya Ijumaa ili kuruhusu kufanyika kwa shughuli ya kupuliza dawa za kuua viini.
Katika notisi iliyochapishwa leo hii, msajili huyo ametangaza kwamba shughuli hiyo itafanyika Ijumaa na Jumamosi kisha mahakama kufunguliwa Jumatatu.
Kulingana na notisi hiyo, hatua ya kupuliza dawa ni mojawapo ya juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona na kuwalinda wanaotumia mahakama.
Mwaka uliopita Mahakama ya Milimani ilifungwa kwa siku 14 baada ya afisa mmoja anayehudumu katika mahakama hiyo kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya korona. Kufikia jana idadi jumla ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona ilikuwa watu elfu mia moja na mia moja tisini na watatu.
Share this: