
Imebainika kuwa mzozo wa ardhi ndiyo sababu ya mwanaume mwenye umri wa miaka sabini kuwaua wazazi wake wakongwe kwa kuwakata kwa upanga na kuwadunga kisu mapema leo alfajiri kwenye eneo la Mukaa katika Kaunti ya Makueni.
Kamanda wa Polisi wa Makueni, Joseph Ole Napeiyan amesema amepokea taarifa kuhusu tukio hilo ambapo, mshukiwa John Nzingu Ndivo amemkata kichwani babaye Ndivo Ndolo mwenye umri wa miaka 96 na mamaye Kamumbi Ndivo mwenye umri wa miaka 86.
Polisi wamemkamata mwanaume huyo aliyekuwa pia na majeraha ya kisu shingoni huku akiwa na upanga na kisu.
Mili ya wazazi wake imepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Kilungu uchunguzi zaidi ukiendelea.
Share this: