
Kauli ya Rais Uhuru Kenyatta kwamba uongozi wa taifa hili unapaswa kuwachiwa makabila mengine imeendelea kuibua hisia kinzani.
Kinara wa ODM Raila Odinga amerejelea kuunga mkono matamshi hayo akisema kwamba wakati uemwadia kwa makabila mengine kutwaa wadhifa huo ili kuendelea moyo wa umoja na utangamano.
Akihojiwa na runinga mmoja humu nchini mapema leo, Raila ametoa mfano wa mataifa ya Nigeria na Uswizi ambayo yamekuwa yakiendeleza mfumo huo wa urais unaogawanywa kwa makabila mbalimbali.
Share this: