
Mshukiwa Mkuu wa mauaji ya watu watano wa familia yake katika eneo la Kiambaa kwenye Kaunti Kiambu Lawrence Warunge na mpenziwe wanatarajiwa kufikishwa mawakamani adhuhuri hii kufunguliwa mashataka ya mauaji.
Warunge ambaye alikiri kuwaua jamaa zake tayari amethibitishwa kuwa mwenye akili timamu.
Upande wa Mashtaka katika kesi hiyo ulikuwa umeomba muda wa majuma mawili ili kukamilisha uchunguzi wake.
Mahakama sasa inatarajiwa kuanza vikao vya kumwajibisha Warunge ambaye aliwaua kinyama baba na mama yake, kaka yake, binamuye na mfanyakazi wao tarehe Januari tarehe 9 .
Share this: