
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko ameendeleza shutma dhidi ya serikali wakati huu akidai kwamba inafanya kila iwezalo kulipaka tope mrengo wa Tangatanga.
Sonko ambaye ameonekana kujawa na hamaki amedai kwamba serikali ilihusika kupanga na kufadhili rabsha zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
Sonko amekuwa akiikosoa serikali katika mikutano ya hadhara baada ya yeye kutimuliwa kutoka wadhifa wa ugavana kufuatia kesi iliyowasilishwa dhidi yake
Share this: