
Mahakama Kuu Nchini Uganda imewaagiza maafisa wa polisi na wananjeshi nchini huko kuondoka nyumbani kwa mwanasiasa Bobi Wine.
Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama hiyo mapema leo, kuendelea kuzuiliwa kwa mwanasaisa huyo wa upinzani ni ukiukaji mkubwa wa sheria na Katiba ya Uganda.
Wine ambaye majina yake halisi ni Robert Kyagulanyi, amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake eneo la Magere baada ya uchaguzi wa urais ambapo Yoweri Museveni alichaguliwa kuhudumu kwa awamu ya 6.
Share this: