
Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema kwamba watahiniwa wote wa mtihaniwa wa Darasa la Nane watapewa vitambaa vya hedhi kwa muda wa miezi mitatu. Vitambaa hivyo vitasambazwa kupitia ushirikiano wa Wakfa wa Mpesa na Wizara ya Elimu.
Wakfu wa Mpesa umetoa vitambaa 540,000 ambavyo vitawafaidi wasichana 188,000 kwenye mitaa ya mabanda na familia zisizojiewa.
Waziri Magoha amezungumza katika Tasisi y Ukuzaji Mtalaa KICD jijini Nairobi ambapo amezindura rasmi mradi huo.
Afisa Mkuu Mtendadhi wa Wakfu wa Mpesa Michael Joseph, amesema ukosefu wa vitambaa hivyo umewaweka wasichana katika hatari ya kudhulumiwa kingono na hivyo basi kuathiri pakubwa masomo yao.
Mradi huo wa kuwanufaisha wasichana na vitambaa vya hedhi ulianzishwa na serikali mwaka wa 2017
Share this: