×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shule ya Wavulana ya Chesamisi imefungwa baada ya wanafunzi kugoma

Shule ya Wavulana ya Chesamisi imefungwa baada ya wanafunzi kugoma

Shule ya Upili ya Wavulana ya Chesamisi, kwenye Kaunti ya Bungoma imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia mgomo wa wanafunzi.

Mgomo huo uliofanywa usiku wa kuamkia leo umechangia kuharibiwa kwa mali yenye thamani isiyojulikana.
Kulingana na baadhi ya wanafunzi, mgomo huo ulisababishwa na uongozi wa kiimla kutoka kwa Naibu Mwalimu Mkuu kwa jina Tom Adanga.

Wanafunzi hao wamemlaumu Adanga kwa kubadilisha ratiba ya kuvinjari shuleni humo kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa nne usiku muda wa kawaida hadi kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christopher Serem amesema uchunguzi utaanzishwa kufuatia mgomo huo na shule hiyo itaamua adhabu itakayopewa wanafunzi hao.

Washikadau katika sekta ya elimu wakiongozwa na George Okoth amesikitishwa na hatua ya wanafunzi hao ila akawataka kusalia watulivu.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Bungoma, Musyoki Mutungi ambaye amesema baadhi ya wanafunzi hao wamepotoka kimaadili. Amesema wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Share this: