
Watu wengine themanini na watano wameambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.
Idadi hii imetokana na sampuli elfu mbili mia tisa themanini na tano zilizopimwa katika kipindi hicho, kumaanisha kwamba viwango vya maambukizi leo hii ni asilimia 2.8.
Jumla ya watu walioambukziwa korona nchini ni elfu tisini na tisa mia tisa themanini na tatu.
Wakati uo huo, waliopona ni thelathini na watatu na kufkisha jumla kuwa elfu themanini na mbili mia tisa sitini na tisa.
Wagonjwa wengine wanne wamefariki dunia, hivyo jumla ni elfu moja mia saba arubaini na wanne.
Share this: