
Viwango vya maambukizi ya Korona vimeendelea kuwa chini ya asilimia 5, ambapo tarehe 23 Januari imekuwa asilimia 2. 5 sawa na ilivyorekodiwa siku iliyotangulia.
Vilevile, hakuna mtu ambaye ameripotiwa kufariki dunia leo hii kutokana na Ugonjwa wa COVID-19, hivyo idadi jumla ya waliofariki kutokana na Korona kusalia kuwa 1, 740.
Hata hivyo, watu 129 wamethibitishwa kuambukizwa Virusi vya Korona, katika saa 24 zilizopita, hivyo kufikisha jumla ya visa vya maambukizi nchini kuwa 99, 898.
Takwimu hizo zimetokana na vipimo vya sampuli 5, 091.
Nairobi imeendelea kuongozwa kwa wingi wa idadi ya waliambukizwa ambao ni 81, Kiambu 8, Mombasa 8, Siaya 7, Nakuru 5, Kajiado 4, Kilifi 4, Uasin Gishu 3 na Kitui 3.
Aidha, wagonjwa 70 wamethibitishwa kupona, na kufikisha jumla ya waliopona kuwa elfu 82, 936
Share this: