
Mbunge wa Alego Usonga, Samuel Atandi amemshtumu Naibu wa Rais, William Ruto kufuatia kauli yake kwamba mapungufu yanayoshuhudiwa serikalini yamesababishwa na Chama cha ODM.
Akihutubu katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Ndhiwa, Owigo Olang, Atandi badala yake amesema mkwamo wa miradi ya maendeleo umesababishwa na Ruto.
Atandi amesema serikali ya Jubilee imeshindwa kutekeleza ahadi kwa Wakenya hivyo Ruto hapaswi kumlaumu Kinara wao Raila Odinga baada ya kuungana na Rais Uhuru Kenyatta.
Awali Ruto aliishtumu ODM akisema imechangia kutotekelezwa kwa maendeleo serikalini kwa kuwa imefanya kipaumbele siasa badala ya ajenda nne kuu za serikali.
Pia aliishtumu ODM kwa madai ya kusambaratisha Jubilee.
Share this: