
Viongozi wa eneo la Mlima Kenya wanazidi kushinikiza mazungumzo kufanyika kuhusu mpango wa BBI kabla ya kufanyika kwa kura ya maamuzi.
Wa hivi punde ni Kiongozi wa Chama cha the Service Party Mwangi Kiunjuri, ambaye amesema japo anaunga mkono BBI, aoni ya Wakenya wote sharti yasikilizwe.
Akizungumza baada ya mkutano wa wanachama jijini Nairobi leo hii, Kiunjuri amesema ni kupitia mazungumzo tu ndipo changamoto zinazowakabili Wakenya zinaweza kushughulikiwa.
Share this: