
Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang'i ameendelea kuwaonya wanasiasa wanaochochea ghasia kwenye eneo la Kapedo katika Mpaka wa Turkana na Baringo.
Akizungumza katika eneo la Ebogogo, kwenye Kaunti ya Kisii Waziri Matiang'i amesema kwa miaka mingi wanasiasa wamekuwa wakichochea wizi wa vifugo hali ambayo imesababisha mauaji ya watu wengi
Matiang'i amepuuza wito wa baadhi ya viongozi wanaotaka oparesheni ya kiusalama inayoendelea kusitishwa, akisema itaendelea hadi washukiwa wote watakaponaswa.
Siku iliyotangulia, Mshirikishi wa Utawala wa eneo la Bonde la Ufa George Natembeya alisema uchungizi unaedelea dhidi ya baadhi ya wabunge na wawakilishi wadi wanaoaminika kuchochea ghasia kwenye eneo hilo.
Share this: