×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamume amuua rafiki na kuteketeza mwili wake kwa sababu ya deni

Mwanamume amuua rafiki na kuteketeza mwili wake kwa sababu ya deni

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wanamzuilia mwanaume wa miaka 29 aliyemuua rafiki yake kisha kuteketeza mwili wake katika eneo la Nzombi kwenye kaunti ya Kitui.

Inaarifiwa Nicholas Luka alitekeleza mauaji hayo kutokana na deni la shilingi 4, 000.

Kulingana na DCI Luka ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji hayo yaliyotekelezwa tarehe 13 mwezi Januari 2019.

Inaarifiwa marehemu Simon Mwangangi mwenye umri wa miaka thelathini na sita alizozana na rafiki yake na walipokosa kuelewana mshukiwa alimuua kwa kumkata kwa upanga shingoni.

Baadaye aliubeba mwili huo akitumia karatasi za plastiki hadi kichaka kilichokuwa karibu ambapo aliuteketeza.

Polisi kwa ushirikiana na nduguye marehemu ndio walioyapata mabaki ya mwili huo kichakani humo kufuatia msako mkali.

Share this: