
Kiongozi wa KANU Gideon Moi ameendeleza kampeni za Mpango wa BBI ambao leo hii amezuri kaunti ya Laikipia, na kuwahimiza Wakenya kujiepusha na wanasiasa wanaoeneza propaganda kuhusu BBI.
Akiwahutubia wananchi katika eneo la Rumuruti, Moi ambaye pia ni Seneta wa Baringo amekariri haja ya wananchi kujiamulia watakacho bila kutegemea propaganda.
Amewakashifu viongozi wanaopinga BBI akisema wanafanya hivyo kwa malengo ya binafsi.
Wakati uo huo, Seneta Moi amesisitiza haja ya Rais Uhuru Kenyatta kuheshimiwa kwa kuwa kiongozi wa taifa, akiwakosoa wanasiasa wanaomtusi Rais kwa lengo la kujitafutia umaarufu
Share this: