
Na Mate Tongola,
NAIROBI, KENYA, Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya korona nchini sasa inakaribia kufika laki moja baada ya watu 139 zaidi kuripotiwa kuambukizwa chini ya saa 24 zilizopita kutokana na sampuli 5,487.
Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa idadi ya maambukizi huku 119 miongoni mwa 139 walioambukizwa wakiwa ni raia wa Kenya, mdogo zaidi akiwa mtoto wa umri wa miaka mili huku mzee zaidi akiwa na miaka 85.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, wagonjwa 137 waliokuwa wakiugua Covid-19 wameripotiwa kupona, 110 miongoni mwao wakiwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku 27 wakiwa waliokuwa mayumbani.
Hata hivyo, mgonjwa mmoja amefariki dunia na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 1,740.
Kwa sasa, kiwango cha maambukizi ni 2.5 ikilinganishwa na jana ambapo ilikuwa 2.3.
Share this: