×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Kalonzo ajiwasilisha DCI

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Maafisa wa Idara ya Upelelezi wamemhoji Kinara wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka baada ya yeye kujiwasilisha kuhojiwa kuhusu madai ya unyakuzi wa ardhi katika eneo la Yatta kwenye Kaunti ya  Machakos. 

Kalonzo amewasili huko akiwa ameandamana na viongozi kadhaa akiwamo Wakili wake James Orengo huku akiwa na stakabadhi muhimu za kuonesha uhalali wa umiliki wake wa ardhi ya Yatta katika Kaunti ya Machakos anayodaiwa kunyakua.

Kalonzo amesema anawasilisha vyeti hivyo vya kuonesha aliyemuuzia ardhi hiyo na jinsi alivyoinunua, kinyume na alivyodai Naibu Rais William Ruto kuwa aliinyakua kutoka kwa Taasisi ya Huduma za Vijana NYS ya Yatta.

Katika hotuba yake mapema wiki hii, Kalonzo alimtaka Ruto kuweka wazi vyeti vya umiliki wa sehemu zake za ardhi anazodaiwa kunyakua. Aidha, amemtaka Ruto pia kujiwasilisha kurekodi taarifa kuhusu madai hayo.

Share this: