×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hali yazidi kuwa tete eneo la Kapedo

Hali yazidi kuwa tete eneo la Kapedo

Na Beatrice Maganga,

NAIROBI, KENYA, Taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Kapedo kwenye Kaunti ya Baringo baada ya mkuu mwingine wa polisi na dereva wake kuuliwa kwa kupigwa risasi na washukiwa wa ujambazi jana jioni. 

Kamanda wa Polisi anayekisimamia kitengo cha polisi wa kushughulikia hali za dharura, RDU alivamiwa pamoja na dereva wake ambaye pia ni afisa wa polisi katika daraja la Ameyan kwenye Eneo Bunge la Tiaty. Raia mmoja pia alijeruhiwa wakati wa kisa hicho.

Mshirikishi wa Utawala katika eneo la Bonde la Ufa, George Natembeya amesema mkuu huyo wa polisi anayezisimamia kambi za Lomelo na Kapedo alikuwa akirejea kazini baada ya kuhudhuria hafla ya mazishi ya mamake.

Tukio hilo lilifanyika karibu na lile la juzi ambapo Mkuu wa GSU katika eneo hilo, Emadau Tebakol aliuliwa kwa kupigwa risasi na wavamizi. Hizi hapa kauli za baadhi ya wakazi wakilalamikia utovu wa usalama.

Maafisa wa usalama wamekuwa wakiendeleza oparesheni kali tangu kuuliwa kwa mkuu huyo wa polisi huku mili ya watu sita ikipatikana takriban kilomita 129 kutoka Kapedo ambako mavamizi yamekuwa yakifanyika.

 Inadaiwa kwamba watu hao waliokuwa katika baa kwenye eneo la Chemolingot walinaswa na watu wasiojulikana na baadaye kupatikana wakiwa wameuliwa. Miongoni mwa waliouliwa ni afisa wa Tume ya Uchaguzi, IEBC.

Hayo yanajiri huku Mbunge wa Tiaty, William Kamket  akiagizwa kufika katika ofisi za Idara ya Upelelezi, DCI kwenye Kaunti ya Nakuru siku ya Alhamisi wiki ijayo. Kamket alikamatwa jana na kuhojiwa kuhusu suala la utovu wa usalama katika eneo la Kapedo kabla ya kuachiliwa huru. 

Akizungumza baada ya kuachiliwa, Kamket alikosoa namna operesheni ya kiusalama inayoendelezwa katika eneo la Kapedo akisisitiza haja ya serikali kubadili mbinu ya kukabili shida iliyopo.

Kamket anahusishwa na mapigano vilevile wizi wa mifugo katika eneo la Kapedo, Baringo ambapo operesheni kali inaendelea kutekelezwa.

Share this: