×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kesi za kupinga BBI kuanza kusikilizwa

Kesi za kupinga BBI kuanza kusikilizwa

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Kesi saba zilizowasilishwa mahakamani kupinga marekebisho ya katiba kupitia mpango wa BBI zitasikilizwa kati ya tarehe 17 na 19 Machi mwaka huu.

Miongoni mwa kesi hizo ni ile iliyowasilishwa na Chama cha Kitaifa cha Wauguzi KNUN, ile iliyowasilishwa na mwanasheria Mkuu wa Serikali Kihara Kariuki ile iliyowasilishwa na Chama cha Thirdway Alliance miongoni mwa nyingine.

Aidha Mahakama Kuu imekataa ombi lililowasilishwa mahakamani kutaka Tume ya Uchaguzi IEBC kusitisha mpango wa kuthibitisha saini zilizowasilishwa na kamati tendaji ya BBI ili kufanikisha mpango huo.

Hayo yanajiri wakati IEBC imechapisha majina ya waliosaini huku ikiwashauri kuthibitisha iwapo waliorodheshwa kuunga mkono BBI bila idhini yao kabla ya orodha ya mwisho kutolewa .

Kulingana na orodha hiyo IEBC imethibitisha takriban saini milioni 1.3 huku ikisema shughuli hiyo ingali inaedneelea. Tume hiyo imesema baada ya shughuli nzima kukamilika mswada huo  utawasilishwa katika Mabunge ya Kaunti ili kupisha mchakato wa kufanyika kura ya maamuzi.

Kulingana na katiba sharti mswada huo uungwe mkono na mabunge 24 na zaidi kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

Share this: