×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Biden akabidhiwa mamlaka ya uongozi huku Trump akisifu utendakazi wake akiwa madarakani

Biden akabidhiwa mamlaka ya uongozi huku Trump akisifu utendakazi wake akiwa madarakani

Rais wa Marekani anayeondoka Donald Trump ametoa hotuba yake ya mwisho dakika chache tu baada ya kuondoka Ikulu ya White House kupisha hafla ya kuapishwa kwa mrithi wake Joe Biden.

Trump ametumia fursa hiyo kuendelea kupigia debe uongozi wake, akisema alibuni nafasi nyingi za kazi japo mpango huo uliathiriwa pakubwa na janga la virusi vya korona.

Licha ya kuwa Marekani ndiyo imerekodi idadi ya juu zaidi ya watu ambao wamefariki dunia kutokana na korona, amedai jinsi alivyoshughulikia vyema janga hilo, akisema ni utawala wake ndio uliochangia kuharakishwa kupatikana kwa chanjo dhidi ya virusi hivyo.

Trump ambaye alipinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana amewahakikishai wafuasi wake kwamba atarejea. Awali Rais Trump ameondoka katika Ikulu ya White House akiwa  ameandamana na mkewe Malania Trump.

Trump hatahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Biden huku waliokuwa Marais Barack Obama, George W.  Bush na Bill Clinton wakitarajiwa kuhudhuria. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka mia moja ambapo rais anayeondoka amesusia kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa mrithi wake. Mara ya mwisho hilo lilifanyika ilikuwa mwaka 1869

Hata hivyo imebainika kwamba Trump alimwachia barua Biden katika Ikulu kabla ya kuondoka.

Share this: