
Chama cha ODM kimeanza rasmi mikakati ya kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao mwaka 2022 na kumtafuta mgombeaji wake wa urais.
Bodi ya Uchaguzi ya ODM imetakiwa kuwaalika wote walio na nia ya kukitumia chama hicho kuwania urais huku tangazo lilikitarajiwa kuchapishwa hivi karibuni.
Miongoni mwa maafikiano mengine ya mkutano uliongozwa na Kinara wa ODM, Raila Odinga ni kufufua matawi ya chama hicho mashinani na kujazwa kwa nafasi zote zilizo wazi.
Chama hicho pia kimesisitiza kuhusu kuhusishwa kwa usimamizi wake katika mazungumzo yote na vyama vingine huku kikitaja hali ambapo Naibu Gavana Mteule wa Nyamira aliyependekezwa na chama, James Gesami alikataliwa kuwa ishara ya kutofuatwa kwa taratibu.
Chama hicho trayari kimependekeza jina jingine japo hakijataja ni nani.
Tofauti na mikutano yake ya kawaida ODM leo hii haijazungumzia suala la BBI huku Raila Odinga aliyehudhuria mkutano huo hakuhutubu na kumpa Sifuna jukumu hilo.
Share this: