×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Washukiwa wa Al Shabaab waharibu mtambo wa mawasiliano Mandera

Washukiwa wa Al Shabaab waharibu mtambo wa mawasiliano Mandera

Watu wanaoshukiwa kuwa magaidi wa Al- Shabaab wamevamia eneo la Sarman kwenye Kaunti ya Mandera na kuharibu mtambo wa mawasiliano.

Wakazi wanasema kwamba watu zaidi ya hamsini wamevamia eneo hilo usiku wa kuamkia leo huku mawasiliano yakitatizika.

Kupitia mtandao wake wa twitter, Gavana wa Mandera Ali Roba amesema kwamba kisa hicho kimetoka yapata kilomita mia mbili kutoka mpaka wa Somalia.

Kisa hiki kimejiri huku eneo hilo likikumbwa na misururu ya mashambulizi ya kigaidi ambapo watu watatu wameuliwa, wengine wasijulikane waliko na mali kuharibiwa.

Kauli ya Roba imejiri huku serikali ikikupuuza tetesi kwamba magaidi wa Al Shabaab wamezagaa kwenye zaidi ya asilimia 70 ya Kaunti ya Mandera.

Serikali badala yake imewahusisha viongozi wa kisiasa na utovu wa usalama huku operesheni ya kutwaa silaha haramu ikianza leo kwenye Kaunti za Wajir, Garissa na Isiolo.

Katika eneo la Pwani, Mshirikishi wa Usalama - John Elung'ata amewaagiza maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza viongozi ambao wanasemekana kuchochea mzozo uliosababisha kifo cha mtu mmoja katika eneo la Madogo huko Tana River.

 

Share this: