
Rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuapishwa leo jijini Washington kuwa Rais wa 46 wa taifa hilo.
Hata hivyo, Rais anayeondoka Donald Trump anatarajiwa kususia hafla hiyo ambayo itafanyika mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki.
Trump ambaye hajaonekana hadharani kwa kipindi cha wiki moja sasa, amewahutubia wafuasi wake kupitia hotuba iliyorekodiwa kwenye kanda ya video huku akiitakia mafanikio serikali ya Biden.
Wakati uo huo, Trump ameelezea kusikitishwa na ghasia zilizozuka jijini Washington DC wiki mbili zilizopita huku akipigia upatu utawala wake wa miaka minne kwa kufanikisha masuala kadhaa, ikiwamo kuimarisha uchumi wa Marekani, kutia saini mikataba ya amani na Mataifa ya Kaskazini Mashariki na kadhalika.
Share this: