×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakazi wa Kapedo wahama makazi yao wakihofia oparesheni ya kiusalama kufuatia mauaji ya afisa wa GSU

Wakazi wa Kapedo wahama makazi yao wakihofia oparesheni ya kiusalama kufuatia mauaji ya afisa wa GSU

Mamia ya wakazi wa Kapedo na maeneo jirani katika Kaunti ya Turkana wameanza kuhama makazi yao wakihofia usalama wao kufuatia oparesheni ya kiusalama inayondeshwa eneo hilo kuwakabili wezi wa mifugo ambao walimuua afisa wa GSU wa ngazi ya juu wiki hii.

Aidha, shughuli za masomo zimesitishwa kufuatia kufungwa kwa baadhi ya shule walimu wakihofia usalama wao.

Taharuki inazidi kutanda huku Oparesheni kali ya kuwapokonya silaha wakazi wa Kaunti za Wajiri, Garissa na Isiolo ikitarajiwa kufanyika hivi karibuni kufuatia visa vya utovu wa usalama.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi Dakta Fred Matiang'i,  ametoa onyo kali kwa viongozi wa maeneo hayo anaosema wanahusika katika kuyapa ufadhili makundi haramu ya vijana ambayo yamekuwa yakitekeleza wizi, kuharibu mali na kuwauwa watu.

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa eneo hilo, Matiang'i amewataka waliohusika na mauaji ya afisa huyo wa jeshi kujisalimisha kabla ya operesheni hiyo. Matiang'i pia amevituhumu baadhi ya vyombo vya habari vya sehemu hizo kwa kuchochea mapigano mpakani.

Share this: