×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Atwoli atishia kuitisha mgomo wa wafanyakazi wote nchini

Atwoli atishia kuitisha mgomo wa wafanyakazi wote nchini

Huenda mgomo wa wahudumu wa afya ukachukua mkondo mpya baada ya Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli kutishia kuwashinikiza wafanyakazi wote kugoma.

Katika mahojiano na Runinga ya KTN NEWS, Atwoli amesema hatua hiyo inalenga kushinikiza serikali kutekeleza matakwa ya wahudumu wa afya ambao wamekuwa kwenye mgomo kwa wiki ya saba sasa.

Aidha, amewaonya magavana dhidi ya kuwafuta kazi wahudumu wa afya wanaogoma na badala yake kuwataka watafute suluhu ya mgomo huo.

Hayo yanajiri huku Maafisa wa Kliniki, Wauguzi na Maabara kwenye Kaunti ya Mombasa wakitaka kutoa takwa jingine la kutaka kupandishwa vyeo.

Katibu wa Chama cha Wauguzi tawi la Mombasa, Peter Maroko amesema kwamba baadhi ya wahudumu hawajapandishwa vyeo tangu mwezi wa Juni mwaka uliopita jinsi ilivyoahidi serikali ya kaunti.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Maafisa wa Kliniki, Franklin Makanga amemshtumu Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wycliffe Oparanya kwa kuliingiza siasa suala la mgomo wao.

Ijumaa wiki iliyopita, Serikali ya Kaunti ya Mombasa ilitia saini mkataba wa makubaliano wa kurejea kazini na Chama cha Madaktari, KMPDU bila kuwaangazia wahudumu wengine wa afya.

Share this: