×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mazungumzo ya biashara huru baina ya Kenya na Marekani kukamilika hivi karibuni

Mazungumzo ya biashara huru baina ya Kenya na Marekani kukamilika hivi karibuni

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza msimamo wake wa kukamilisha mazungumzo ya kusaini mkataba wa maelewamo ya biashara huru na Marekani.

Akitoa hakikisho hilo kwa Balozi wa Marekani humu nchini anayeondoka ofisini Kyle McCarter, Kenyatta amesema mkataba huo utachangia kukua kiuchumi kwa mataifa haya mawili kwa kubuni nafasi zaidi za ajira na uwekezaji.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika Ikulu, Kenyatta aidha amempongeza Balozi MacCarter kwa ushirikiano wake na serikali ya Kenya tangu alipoanza kutekeleza majukumu yake hapa nchini.

Kenya na Marekani zilizindua mazungumzo hayo ya kibiashara tarehe 8 mwezi Julai mwaka 2020, lengo likiwa kuimarisha uchumi wa mataifa haya vilevile wa Bara la Afrika.

Kenyatta aidha ametambua juhudi za Marekani katika kuisaidia Kenya kwenye Sekta ya Usalama hasa kwa kuwakabili magaidi wa Al Shabaab vilevile ilivyokuwa mustari wa mbele katika kukabili maambukizi ya korona.

Kwa upande wake Balozi MacCarter amemhakikishia Kenyatta kwamba mazungumzo yote yaliyoafikiwa baina ya serikali hizi mbili yatatekelezwa kikamilifu.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua na Waziri wa Mambo ya Nje Raychelle Omamo.

Share this: