×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Said Chitembwe kuongoza vikao vya kumwondoa mamlakani Philomena Mwili

Said Chitembwe kuongoza vikao vya kumwondoa mamlakani Philomena Mwili

Vikao vya kusikiliza kesi ya kumwondoa mamlakani Kaimu Jaji Mkuu, Philomena Mwili vitafanyika tarehe 18 na 19 Februari mwaka huu.

Jaji wa Mahakama Kuu, Said Chitembwe ataongoza jopo la majaji watatu linalowajumuisha majaji Weldon Korir na Roselyn Aburili kusikiliza kesi dhidi ya Mwilu.

Agosti tarehe 14 mwaka uliopita Mwilu alipokea agizo la mahakama kusitisha kusikilizwa kwa kesi dhidi yake na Tume ya Huduma za Mahakama, JSC kwa misingi kwamba makamishna wawili; Kihara Kariuki na Macharia Njeru walikuwa wakiegemea upande mmoja.

JSC ilifutulia mbali madai yake na kumlazimu kuelekea katika Mahakama ya Kuu ambayo ilizuia kufanyika kwa shughuli hiyo.

Hata hivyo, Msajili wa Idara ya Mahakama Ann Amadi ameitaka mahakama kufutulia mbali malalamiko ya Mwilu kutaka kesi yake kutosikilizwa akisema hayana misingi.

Mwilu anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya mamlaka na kughushi stakabadhi. 

Share this: