
Wauguzi wameapa kuendelea na mgomo wao ambao umeingia wiki ya saba leo hii hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa kikamilifu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi KNUN Seth Panyako na Naibu wake Maurice Opetu wamesisitiza kwamba masuala ya bima ya afya, nyongeza ya mishara vilevile marupurupu ni sharti yatekelezwe.
Kwenye kikao na wanahabari, viongozi hao aidha wamewalaumu Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Wycliffe Oparanya na Waziri wa Leba Simon Chelugui kwa kulemaza juhudi za kutatua mgomo wao.
Wakati uo huo Panyako amerejelea kauli yake ya kutaka kujumuishwa kwa pendekezo la kubuniwa kwa Tume ya Huduma za Afya katika ripoti ya Mpango wa Upatanishi BBI. Amesema iwapo hilo litazingatiwa basi wahudumu wote wa afya watakuwa mstari wa mbele kufanikisha Mswada wa Kura ya Maamuzi wa Mwaka 2020.
Kauli ya KNUN inajiri huku, Gavana Oparanya akiwaandika kazi wahudumu wa afya kadhaa watakaohudumu kwa muda huku wahudumu takribani mia tano kwenye Kaunti ya Taita Taveta wakifutwa kazi kwa kushiriki mgomo huo.
Share this: