×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

65 waambukizwa, 77 wapona, 3 wafariki

65 waambukizwa, 77 wapona, 3 wafariki

Idadi ya maambukizi ya virusi vya korona inazidi kupungua, leo hii watu sitini na watano wakiambukizwa kutokana na sampuli elfu mbili, mia sita themanini na moja.

Hadi sasa jumla ya maambukizi imefikia watu elfu tisini na tisa, mia mbili ishirini na saba kote nchini.

Viwango vya maambukizi ni aslimia 2.4 kulinganishwa na jana ambapo vilikuwa asilimia 2.1.

Aidha wagonjwa wengine wa Covid-19 mia sita tisini na saba walazwa kwenye hospitali mbalimbali huku elfu moja mia sita na themanini wakihudumiwa nyumbani. Ishirini na wanane wamelazwa ICU na mmoja akihitaji uangalizi wa karibu.

Wakati uo huo, wagonjwa wengine sabini na saba wamepona Covid-19. Wagonjwa sitini walikuwa wakihudumiwa nyumbani na kumi na saba kwenye vituo vya afya. Kwa jumla waliopona ugonjwa huo hatari ni elfu themanini na mbili, mia nne ishirini na saba.

Hata hivyo, wagonjwa wengine watatu wamefariki na kufikisha jumla ya walioaga kuwa elfu moja, mia saba thelathini na wanne.

Share this: