
Kinara wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka amemshauri Naibu wa Rais William Ruto kujiwasilisha kwa polisi kufanyiwa uchunguzi kuhusu sakata mbalimbali za wizi wa mali ya umma.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Kalonzo aidha amemtaka Ruto kuweka wazi mali anazomiliki akisema kwamba alizipata kutokana na kashfa za ufisadi.
Musyoka amemkashifu Ruto kwa kijipendekeza kuwa mtetezi wa umma ilhali amelenga kujinufaisha
Share this: