×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Taharuki yatanda Kapedo baada ya kuuliwa kwa Afisa wa GSU

Taharuki yatanda Kapedo baada ya kuuliwa kwa Afisa wa GSU

Taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Kapedo kwenye Kaunti ya Turkana kufuatia operesheni kali ya vikosi vya usalama dhidi ya wezi wa mifugo.

Makabiliano makali yanaendelea kufuatia kifo cha naibu afisa mkuu wa oparesheni kwenye kitengo cha polisi cha GSU ambaye alipigwa risasi na kuuliwa na wezi hao hapo jana  

Wakati wa oparesheni hiyo watu kadhaa walijeruhiwa vibaya walipokuwa kwenye msafara wa magari kuelekea eneo la Ameyen.

Wabunge watatu wa Turkana ambao walikuwa wamezuru eneo hilo kuzifariji familia za watu walioshambuliwa hivi majuzi wameshindwa kutoka Kapedo kwani barabara zote hazipitiki.

Watatu hao ni James Lomenen wa Turkana kusini, Ali Lokiru wa Turkana mashariki na John Lodepe wa Turkana ya Kati.

Aidha inadaiwa kuwa raia watatu waliuliwa wakati wa makabiliano makali ya jana.

Inspekta Mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai, tayari amethibitisha kuwapo kwa oparesheni hiyo huku akiwahakikishia wananchi kwamba wahusika watakamatwa.

Share this: