×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais akiri kuna ufisadi serikalini

Rais akiri kuna ufisadi serikalini

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine amekiri kukithiri kwa ufisadi katika serikali yake.

Akihojiwa katika baadhi ya redio zinazotangaza kwa lugha ya Kikuyu mapema leo, Uhuru amesema kwamba Kenya hupoteza zaidi ya shilingi bilioni 2 kila siku kupitia ufisadi.

Kenyatta ambaye ametetea suala la mabilioni ya fedha kutumiwa kufanikisha kura ya maamuzi, amesema kwamba ni kinaya kwa wanaopinga kutumiwa kwa kiasi hicho cha fedha  ilhali mabilioni ya fedha yanafujwa.

Aidha, Uhuru amesema ni mapema mno kuelezea kiwango cha fedha kitakachohitajika kufanikisha mchakato huo licha ya Tume ya Uchaguzi, IEBC awali kusema kwamba itagharimu shilingi bilioni 14.

Wakati uo huo, Uhuru amemshtumu Naibu wake, William Ruto kwa kutumia kaulimbiu Hustler Nation akisema kwamba huenda hatua hiyo ikawagawanya wananchi hata zaidi.

Share this: