
Ikulu ya rais leo imelazimika kuondoa jumbe ilizotuma kupitia mitandao ya kijamii ambapo Rais Uhuru Kenyatta alipongeza Rais wa Uganda Yoweri Museveni kufuatia ushindi wa urais.
Hatua hiyo inafuatia hatua ya mtandao wa Facebook kusema kwamba ujumbe wa Ikulu wa kumpongeza Museveni haikuwa wa kweli.
Kilichosababisha Facebook kuchukua hatua hiyo ni picha iliyotumika awali katika taarifa ya awali ambayo haikuwa ya kweli kwamba Museveni alikuwa amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Katika ujumbe wa kupongeza Museveni Rais Uhuru Kenyatta alisema kuchaguliwa kwa Museveni kwa muhula wa sita kunaonesha imani ya raia wa Uganda walioyonayo kwa uongozi wake.
Kulingana na Rais Kenyatta chini ya uongozi wa Museveni taifa hilo limesalia imara kando na kuendelea kuimarika kiuchumi.
Museveni aliibuka Mshindi baada ya kupata kura milioni tano, elfu mia nane hamsini na moja, na thelathini na saba ambazo ni asilimia 58. 64 ya jumla ya kura zilizopigwa.
Mpinzani wake mkuu, mwanamziki Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, aliibuka wa pili kwa kupata kura milioni tatu, elfu mia nne sabini na tano, mia tatu tisini na nane ambazo ni asilimia 34. 83 ya kura zote.
Share this: