
Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Kapedo Turkana Mashariki baada ya Afisa Mkuu wa Oprasheni wa Kitengo cha GSU nchini kuuliwa kwa kupigwa na watu wanaoshukiwa kuwa wa Kaunti jirani.
Afisa huyo wa polisi alikuwa amezuru Kapedo mchana wa leo kujadiliana na maafisa wa usalama wa eneo hilo jinsi ya kumaliza uhasama na alipokuwa akirejea Nairobi gari la RDU ambalo alikuwa ameabiri lilishambuliwa katika Daraja la Kapedo kule Ameyan na kuuliwa papo hapo.
Wabunge James Lomenen wa Turkana Kusini, Ali Lokiru wa Turkana Mashariki na John Lodepe wa Turkana ya Kati waliokuwa wamezuru Kapedo kufariji familia za watu walioshambuliwa hivi majuzi wameshindwa kuondoka katika eneo la Kapedo kutokana na hofu ya kuvamiwa.
Share this: