×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sera za Naibu wa Rais ni nzuri, asema Isaac Ruto

Sera za Naibu wa Rais ni nzuri, asema Isaac Ruto

Kinara wa Chama cha CCM, Isaac Ruto amesema hatua yake ya kumuunga mkono Naibu wa Rais, William Ruto ni kutokana na sera zake.

Akihutubu katika eneo la Londiani Kaunti ya Kericho, Ruto amesema amekuwa akisukuma ajenda ya Wakenya wenye tabaka la chini sawa tu Naibu wa Rais.

Amefutilia mbali kauli kwamba anafanya hivyo ili kuchaguliwa tena kuwa Gavana wa Bomet.

Ruto ambaye alikuwa gavana wa kwanza wa Bomet vilevile amemshtumu Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga kufuatia kauli kwamba wakati umefika wa makabila mengine kupewa nafasi ya urais kando na Jamii za Agikuyu na Kalenjin. Kulingana na Ruto, kiongozi huchaguliwa kufuatia maono yake wala si kabila. Amesema kauli ya Rais ambayo iliungwa na Odinga inarejesha nyuma taifa katika siasa zinazotishia amani.

Kauli sawa na hiyo ilitolewa na Mbunge wa Kikuyu, Kimani Ichung'wa ambaye alisema watu wa eneo la Mlima Kenya hawatakubali kuwa watumwa wa siasa za kikabila. 

Share this: