×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

80 waambukizwa korona, 26 wapona, 3 wafariki

80 waambukizwa korona, 26 wapona, 3 wafariki

Idadi ya maambukizi nchini imefikia watu elfu tisini na tisa, mia moja sitini na wawili baada ya watu wengine themanini kuambukizwa katika saa 24 zilizopita.

Maambukizi ya leo yametokana na sampuli elfu tatu, mia saba thelathini na tatu zilizopimwa. Miongoni mwa walioambukizwa; Sitini na wawili ni Wakenya, kumi na wanane wakiwa raia wa kigeni.

Aidha, arubaini na wanane ni wanaume, wanawake wakiwa thelathini na wawili. Mtoto wa miezi kumi na moja na mkongwe wa miaka themanini na moja ni miongoni mwa walioambukizwa virusi hivyo leo hii.

Viwango vya maambukizi leo ni asilimia 2.1.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, idadi ya waliopona Covid-19 imefikia watu elfu themanini na mbili, mia tatu hamsini baada ya watu wengine ishirini na sita kupona ugonjwa huo.

Miongoni mwa waliopona; ishirini na wanne walikuwa wakihudumiwa nyumbani huku wawili wakilazwa hospitalini.

Hata hivyo, wagonjwa wengine watatu wamefariki kufuatia makali ya Covid-19 na kufikisha jumla ya vifo kote nchini kuwa elfu moja, mia saba thelathini na kimoja.

Share this: