×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

ODM imesambaratisha Jubilee, sasa inataka kuondoka' Ruto

ODM imesambaratisha Jubilee, sasa inataka kuondoka' Ruto

Naibu wa Rais, William Ruto amesisitiza kwamba Wakenya hawako tayari kwa siasa za kikabila zinachangia uhasama nchini.

Akizungumza katika eneo la Kipkelion, Kaunti ya Kericho, Ruto aidha ameendeleza shutma dhidi ya viongozi wanaopiga siasa za makabila akisema Wakenya watamchagua kiongozi kulingana na sera zake.

Kadhalika, Ruto amesema Kinara wa ODM, Raila Odinga na wandani wake wana njama ya kusitisha ushirikiano wao na Jubilee baada ya kuisambaratisha ila wameshindwa kufanya hivyo. Amewataka kukoma kumkosoa Rais Uhuru Kenyatta kwamba hajatekeleza miradi ya maendeleo aliyowaahidi Wakenya ilhali ni wao wamechangia kukwama kwa miradi hiyo kwa kuingiza siasa.

Kuhusu kauli ya Odinga kwamba anapaswa kuwaeleza Wakenya kuhusu miradi ambayo amewafanyia Wakenya katika Jubilee, Ruto ameelezea kushangazwa na kauli hiyo akisema ni Odinga na wandani wake hawataki kuipa serikali nafasi ya kutekeleza ajenda zake nne kwa Wakenya. Amesema mradi wa nyumba yenye bei nafuu ingetoa nafasi za ajira kwa vijana ilhali imelemazwa na ODM.

Share this: