
Mwanamme mmoja ambaye ni mfanyabiashara katika Kaunti ya Mombasa amefariki dunia akila uroda kwenye nyumba ya mpenzi wake wa mpango wa kando.
Kulingana na mwanamke huyo, mwanaume huyo alizirai na kufariki dunia papo hapo.
Mwanamke huyo anasema juhudi zake za kuitisha usaidizi kutoka kwa wahudumu wa chumba walichokodi mtaani Chaani, Changamwe ziligonga mwamba.
Tayari polisi wamechukua mwili huo huku uchunguzi ukianzishwa kufuatia kifo hicho.
Share this: